Zaburi 93
Mungu Mfalme 
 1  Bwana anatawala, amejivika utukufu; 
Bwana amejivika utukufu 
tena amejivika nguvu. 
Dunia imewekwa imara, 
haitaondoshwa. 
 2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; 
wewe umekuwako tangu milele. 
 3 Bahari zimeinua, Ee Bwana, 
bahari zimeinua sauti zake; 
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake. 
 4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, 
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: 
Bwana aishiye juu sana ni mkuu. 
 5 Ee Bwana, sheria zako ni imara; 
utakatifu umepamba nyumba yako 
pasipo mwisho.