5
Kumbuka, Yahweh, yaliyo tutokea na uone aibu yetu. Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni; nyumba zetu kwa wageni. Tumekuwa yatima, bila baba, na mama zetu ni kama wajane. Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa, na tulipe fedha kupata mbao zetu. Hao wanakuja kwetu wamekaribia nyuma yetu; tumechoka na hatuwezi pata mapumziko. Tumejitoa kwa Misri na kwa Assiria tupate chakula cha kutosha. Baba zetu walifanya dhambi, na hawapo tena, na tumebeba dhambi zao. Watumwa walitutawala, na hakuna wa kutuokoa na mikono yao. Tunapata mkate wetu pale tunapo hatarisha maisha, kwasababu ya upanga wa nyikani. 10 Ngozi zetu zimekuwa na moto kama jiko kwasababu ya joto la njaa. 11 Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda. 12 Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee. 13 Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni. 14 Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki. 15 Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio. 16 Taji limeanguka kichwani mwetu; ole wetu, kwa kuwa tumetenda dhambi! 17 Kwa kuwa moyo wetu umekuwa unaumwa, na machozi yetu ya fifia, kwa vitu hivi macho yetu yanafifia 18 maana Mlima Sayuni umelala ukiwa, mbwa wa mitaani wacheza juu yake. 19 Lakini wewe, Yahweh, unatawala milele, na utaketi katika kiti chako cha enzi vizazi na vizazi. Kwanini unatusahau milele? 20 Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi? 21 Turejeshe kwako, Yahweh, na sisi tutarejea. Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani - 22 vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi.