| Chapter 5 |
1 | Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi. |
2 | Upendo uongoze maisha yenu, kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzuri na tambiko impendezayo Mungu. |
3 | Kwa vile ninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu. |
4 | Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa. |
5 | Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika Utawala wa Kristo na wa Mungu. |
6 | Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii. |
7 | Basi, msishirikiane nao. |
8 | Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga: |
9 | maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. |
10 | Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana. |
11 | Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya giza bali yafichueni. |
12 | Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. |
13 | Lakini mambo yale yanayotendwa katika mwanga, ukweli wake hudhihirishwa; |
14 | na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: "Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka wafu, naye Kristo atakuangaza." |
15 | Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima. |
16 | Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. |
17 | Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana. |
18 | Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. |
19 | Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. |
20 | Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo. |
21 | Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo. |
22 | Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. |
23 | Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. |
24 | Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote. |
25 | Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. |
26 | Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, |
27 | kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. |
28 | Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. (( |
29 | Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, |
30 | maana sisi ni viungo vya mwili wake.) |
31 | Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja." |
32 | Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. |
33 | Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe. |