Zaburi 23
Bwana Mchungaji Wetu 
Zaburi ya Daudi. 
 1  Bwana ndiye mchungaji wangu, 
sitapungukiwa na kitu. 
 2 Hunilaza katika malisho 
ya majani mabichi, 
kando ya maji matulivu huniongoza, 
 3 hunihuisha nafsi yangu. 
Huniongoza katika njia za haki 
kwa ajili ya jina lake. 
 4 Hata kama nikipita katikati 
ya bonde la uvuli wa mauti, 
sitaogopa mabaya, 
kwa maana wewe upo pamoja nami; 
fimbo yako na mkongojo wako 
vyanifariji. 
 5 Waandaa meza mbele yangu 
machoni pa adui zangu. 
Umenipaka mafuta kichwani pangu, 
kikombe changu kinafurika. 
 6 Hakika wema na upendo vitanifuata 
siku zote za maisha yangu, 
nami nitakaa nyumbani mwa Bwana 
milele.