Zaburi 87
Sifa Za Yerusalemu 
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. 
 1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 
 2  Bwana anayapenda malango ya Sayuni 
kuliko makao yote ya Yakobo. 
 3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, 
ee mji wa Mungu: 
 4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu* Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri. na Babeli 
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: 
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,† Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia. 
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” 
 5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, 
“Huyu na yule walizaliwa humo, 
naye Aliye Juu Sana mwenyewe 
atamwimarisha.” 
 6  Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: 
“Huyu alizaliwa Sayuni.” 
 7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, 
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.” 
*Zaburi 87:4 Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.
†Zaburi 87:4 Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.