Zaburi 110
Bwana Na Mfalme Wake Mteule 
Zaburi ya Daudi. 
 1  Bwana amwambia Bwana wangu: 
“Keti mkono wangu wa kuume, 
mpaka nitakapowafanya adui zako 
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.” 
 2  Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; 
utatawala katikati ya adui zako. 
 3 Askari wako watajitolea kwa hiari 
katika siku yako ya vita. 
Ukiwa umevikwa fahari takatifu, 
kutoka tumbo la mapambazuko 
utapokea umande wa ujana wako.* Au: vijana wako watakujia kama umande. 
 4  Bwana ameapa, 
naye hatabadilisha mawazo yake: 
“Wewe ni kuhani milele, 
kwa mfano wa Melkizedeki.” 
 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume, 
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. 
 6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga 
na kuwaponda watawala wa dunia nzima. 
 7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,† Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka. 
kwa hiyo atainua kichwa chake juu. 
*Zaburi 110:3 Au: vijana wako watakujia kama umande.
†Zaburi 110:7 Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.