Zaburi 131
Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu 
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 
 1 Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, 
macho yangu hayajivuni; 
sijishughulishi na mambo makuu kunizidi 
wala mambo ya ajabu mno kwangu. 
 2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; 
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, 
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya 
ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu. 
 3 Ee Israeli, mtumaini Bwana 
tangu sasa na hata milele.