Zaburi 133
Sifa Za Pendo La Undugu 
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 
 1 Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza 
wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! 
 2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, 
yakitiririka kwenye ndevu, 
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, 
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. 
 3 Ni kama vile umande wa Hermoni 
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. 
Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake, 
naam, hata uzima milele.