Zaburi 134
Wito Wa Kumsifu Mungu 
Wimbo wa kwenda juu. 
 1 Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, 
ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana. 
 2 Inueni mikono yenu katika pale patakatifu 
na kumsifu Bwana. 
 3 Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, 
awabariki kutoka Sayuni.