Zaburi 100
Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu 
Zaburi ya shukrani. 
 1 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote. 
 2 Mwabuduni Bwana kwa furaha; 
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. 
 3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. 
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; 
sisi tu watu wake, 
kondoo wa malisho yake. 
 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani 
na katika nyua zake kwa kusifu, 
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. 
 5 Kwa maana Bwana ni mwema 
na upendo wake wadumu milele; 
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.